Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiliamua kumchukua aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, ajiunge na chama hicho baada ya kubaini katika utafiti maalum uliofanywa na shirika moja kutoka nchi za nje kwamba alikuwa na uwezo wa kubeba asilimia 18 ya kura zote katika uchaguzi mkuu kuliko mgombea mwingine wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita.
Hayo yalizungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakati akihojiwa na Global TV Online ambapo alisema pia Lowassa aliongoza wagombea wote katika utafiti huo.
“Wazungu wakatuambia hivi political personalities zote za Tanzania walimfanyia kila mmoja wao walimfanyia uchunguzi wake, wakatuambia hivi ‘katika wote hao ukimweka huyu na huyu, huyu bwana mkubwa Lowassa huyu yeye peke yake anatembea na asilimia 18 ya Tanzania voters,’ aliyekuwa anamfuata alikuwa na asilimia 11 tu. Kwahiyo Lowassa as Lowassa alikuwa na eighteen percent ya likeability ya kupendwa na hao Watanzania akienda huku anaenda na asilimia 18 ya ziada, akienda huku anaenda na asilimia 18 za ziada nyingine ongezeeni,” alisema Lissu.
“Tukasema hivi, ‘tunataka kushinda uchaguzi eeh tuzungumze na Lowassa’ na Dkt Slaa akasema tuzungumze na Lowassa tukamwambia ‘Dkt una mawasiliano naye’ akasema ‘sina mawasiliano naye, ila kuna mtu ambaye anaweza akawezesha mawasiliano naye ni nani? Askofu Gwajima’ tunaelewana, so this how we got Edward Lowassa.”
No comments:
Post a Comment