AJTC COLLEGE

Monday, 25 September 2017

FUNGUO ZA UFALME

                     







 IBADA YA SIKU YA JUMAPILI  UFUFUO  NA  UZIMA   ARUSHA.
                                                           SNP  FRANK                                 
                         SOMO:     FUNGUO  ZA UFALME          24/9/17.

MATHAYO 16;19
Kwenye serikali ya Mungu tumepewa uwezo wa kufungua lolote na uwezo wa kufungua lolote ufalme wa Mungu upo kwa ajili ya wana wa Mungu ,serikali ipo kwaajili ya kutatua kero  mbalimbali za wanadamu.
Tunaandaa vitu mbalimbali kwaajili ya uchaguzi,pia serikali ipo kwa sababuba ya kutatua kero zao wanaohitaji misaada.
 Pia Mungu nae ana serikali kwaajili ya wana wa mungu kwaajili ya kusaidia kero mbalimbali za watu wa Bwana,wewe unatakiwa upeleke kero kwenye serikali ya Mungu ambayo iko ndani yako,na wewe uliyeokoka unakuwa raia kwenye ufalme wa Mungu.
Ninyi sio raia wa hapa duniani ndio mana mna chukiwa ndio mana hampendwi,kwanini uko jinsi ulivyo kwa sababu ufalme wa Mungu uko ndani yako pia ufunguo wa kufungulia lolote uko ndani yako,watu hatujajua kuutumia ufalme wetu,kwa hiyo wafuga majini wachawi wale wote ni watoto wa giza au wana wa ufalme wa giza,kwa hiyo wanapokuja kumtesa mwana wa Mungu Inakuwa haieleweki,
Sisi watoto wa Mungu tunayomipaka ya kuwaamuru wakuu wa giza ambao hawataweza kuja kwangu bila kukaguliwa mipakani wewe ni raia kwenye serikali ya Mungu ,wachawi hawana mamlaka wakija lazima wauliozwe na walinzi wako ambao ni Malaika watakatifu wa Bwana mana wewe ni raia wa ufalme wa Mungu na kondoo wa malisho yake.
Kuna vitu maalumu ambavyo vimeandaliwa na Bwana  kwaaajili ya wampendao Mungu amewaandalia watoto wake,pia anasema nimekuandalia mambo hapana wa kuzuia ,kwenye ulimwengu war oho kuna stoo ya Baraka za mtoto wa Mungu.
kwa kanuni ya Mungu, Mungu huandaa mahitaji kabla hajamleta mlengwa kwenye mahitaji yake ndio maana Mungu kabla hajamuumba Adamu alianza kwanza kumuandalia mahali ambapo atakuja kuishi.
MWANZO 2:8 na 15 na pia Waefeso 1;3 inazungumzia kuhusiana na Baraka ambazo Bwana ametubarikia
Kule mbinguni kuna chumba cha Baraka  za kila mmoja  ambapo siku ukifika mbinguni utaonyeshwa  na utabaki unashangaa, ni kwanini hapa duniani ulikuwa unahangaika,Yesu anawaambia msisumbukie mle ninyi wala mnywe nini,angalie baba yenu Wa mbinguni anawalisha ndege wa angani ambao hawana hata mashamba wala maghala ya chakula,Je nyinyi si bora kuliko hao ndenge wa angani?
Maombi Pokea funguo za Baraka zako pokea  kwa jina la yesu.
Tatizo sio Mungu tatizo hujafungua wewe mwenyewe,Maisha yako maana Yesu alishatupa unguo wa ufalme lakini watu wengi hawajajua namna ya kuutumia huo ufunguo.
MATHAYO 16:19
Kuna vitu vyako vimefungwa mahali na wakuu wa anga, wakuu wa giza ,mizimu,mashetani,wachawi,waganga wa kienyeji na majeshi ya pepo wabaya kwenye ulimwengu wa roho.
kwenye kila kizazi kinachoendelea kuna waamaleki wanaozuia usiende kwenye Baraka zako,waamaleki ni watoto wa mtu mmoja anaitwa Esau,wana wa Israeli ni watoto wa Yakobo  tunaona watoto wa Esau wamekuwa na vita wanawazuia watoto wa ndugu yake yakobo wasiende kule ambako Mungu alitaka waende kwenye Baraka zao,kile kitendo cha kuwazuia kule Mungu alipotaka waende,tunaona Bwana ameapa atakuwa na vita na waamaleki.
MWANZO 36;16-12
Kuna vita pia inaendelea lazima uinuke kupigana nao,wameshaona mahali unapotakiwa kuingia kwenye Baraka zako.
Kuingia ndani ya Baraka sio tatizo, tatizo hujajua kutumia Baraka zako,ufalme wa Mungu ni kama gari ambalo mtu akifungua anaanza kutumia kuliendesha gari lake,kuna namna ya kufungua na namna ya kutumia hizo barakan zako.
kwenye kufungua Baraka zako lazima upigane vita unapigana ukiwa hapa duniani,Bwana ameapa atakuwa na vita anaefanya vita juu yako Bwana atamfutilia mbali
Bwana akamwambia Musa nina hasira na waamaleki,waamaleki wamesimama kinyume na mapenzi ya Mungu,akamwambia Musa mwambie Yoshua ashuke bondeni akapigane na waamaleki,lazima ushuke mwenyewe  kupigana vita kwaaajili ya Baraka zako,kufungua mlango kunahitaji vita.
KUTOKA  17;8
Waamaleki wakatokea kuwapinga wana wa Mungu ,ule upinzani unaokupinga usiende kwenye Baraka zako ndio vita yako,maisha yana sehemu mbili, unaingia kufungua maisha yako lakini watu  wana kuzuia usiweze kuingia kwenye Baraka zako.
Ufunguo ni mamlaka ya kumpinga shetani ukiwa vitani kwaajili ya kufungua njia pia unatakiwa kuwa mlimani na mikono iwe juu ili ushinde vita,mwamuzi wa kushinda vita kw wana wa Israeli alikuwa  ni Musa  lakini aliyefanikisha huo ushindi alikuwa  Mungu.
Kutoka Misri kwenda Kaanani  ilikuwa ni safari  ya siku tatu lakini wana wa Israeli waliogopa kuipita njia amabayo ingewafikisha kwenye nchi ya ahadi kwa muda wa siku tatu kutokana na kuwa njia hiyo ilikuwa ikikaliwa na wafilisti na badala yake waliamua kupita njia ambayo iliwagharimu miaka arobaini kuifikia nchi ya ahadi .
kuogopa vita unachelewa kufika kwenye nchi yako ambayo Bwana amekuandalia.
MAOMBI ;Katika jina la yesu nakwenda kinyume na wasimamizi wa laana ili usifikie nchi yako ya ahadi kutoka kwa Bwana ninavunjavunja hiyo laana kwa jina la yesu.
Usipopigana itakuchukua muda mrefu kuyafikia mafanikio yako,kuogopa vita na mikono kuwa milegevu ni hatari kwa mafanikio yako,Bwana alimwambia kalebu nimekupa wewe mlima huu uwe urithi wako na watoto wako.
YOSHUA 14;6
Musa akaniapia akisema hakika nchi utakayo kanyaga itakuwa ni nchi yako,kuna Baraka zako zimekaliwa na kiriadhiaba ukiogopa vita unachelewa kumiliki Baraka zako,unapoogopa kupigana vita unachelewesha pia watoto wako .
Vita unayoiogopa kupigana nayo leo watoto wako watakuja kuipigana,usiposhinda vita leo unawapa shida watoto wako.
Kwahiyo unapoogopa kupigana unachelewa kumiliki,tunaona wana wa Israeli walichele kumiliki kwa kuwa njia yao ilikaliwa na wafilisti.
MAOMBI;Kila mfilisti uliyekalia njia yangu  leo nakufuata nakubomoa achia kwa jina la Yesu,ewe kiliadhiaba  unayeshikilia maisha yangu nakuja na ufunguo wa ufalme kuufungua mambo yangu kwa jina la yesu.
Pokea ushindi kwa jina la yesu lazima utengeneze mlango wa Baraka kwa ajili ya uzao wako, miliki ukiwa unanguvu kwa jina la Yesu.
Ukichoka unampa shetani nafasi ya kukupiga
2.SAMWELI 17;1
Mikono ya Daudi ilipochoka Daudi alipigwa.
Mungu amekupa Baraka ila hataki umiliki kizembe,tunaona Adama alipewa bustani ambayo ilikuwa na kila kitu ndani yake lakini Mungu alimwambia  ailime na kuitunza ,maamuzi ya kushinda yako mikononi mwako kuna wakati unatakiwa kwenda kwenye uwanja wa vita na kuna wakati unakuja mlimani.
Kuna pepo la usingizi linakuwa linakuja na kukuletea usingizi wakati unapotaka kuanza kupigana vita yako hivyo ni lazima uwe mkakamavu, usikubali kulala kiroho kwa jina la yesu,ukichoka adui anapanda magugu.
MAOMBI;kila magugu nang’oa  kwa jina la yesu.
Yesu  ametupa  mamlaka  ya kukanyanga  nyoka na ng’e na nguvu zote za Yule muovu ibilisi na hakuna kitakachotudhulu .





  








Thursday, 9 February 2017

Sakata la Dawa ya Kulevya: Askofu Gwajima atema cheche


Gwajima:- Namuomba Rais ambadilishie Kazi Makonda, hii ya Ukuu wa Mkoa kutawala na kuongoza hata watu usiowapenda imemshinda. Sisemi amfukuze hapana nasema ambadilishie Kazi.

Gwajima : Makonda ana chuki na wivu na mimi

Gwajima : alikasirika hata niliposhuka na helkopta yangu siku ya mechi ya viongozi wa dini na wabunge dodoma.

Gwajima : nilichelewa kidogo nikaamua kupanda helkopta yangu mpaka uwanjani kabisa.

Gwajima : mimi nilicheza namba kumi Makonda namba tisa, jicho alilokuwa ananiangalia ni la chuki mpaka nikawa nashangaa.

Gwajima : hii hapa picha niko na Makonda, naibu spika na viongozi wengine tukichangia ujenzi wa taifa mbona hajanikamata hapa kama ninauza unga? .

Gwajima : Makonda alikuja kanisani kwangu na marehemu sitta na akapanda mazabauni je hakujua kama nauza unga? 

Gwajima : hili ni shambulio kwa kanisa sio kwa Gwajima

Gwajima : hili ni shambulio kwa wote walio okoka tuonekane hatufai

Gwajima : hili ni shambulio kwa maaskofu wote na wachungaji wote

Gwajima : kwa sababu Gwajima ana kanisa kubwa

Gwajima : kwa sababu Gwajima ana waumini zaidi ya elf sabini kanisani kwake na makanisa zaidi ya 400 nchi nzima.

Gwajima : nilikuwa mkali Sana kwa serikali ya awamu ya nne na kikwete

Gwajima : nilikemea sana kupotea kwa ndovu kila siku

Gwajima; Makonda anafanya hivi kwa maslahi ya Nani? .

Gwajima : Makonda anafanya hivi kufurahisha serikali iliyopita ionekana nimekomolewa.

Gwajima : Hili ni shambulio kwa Ukristo. Rais wangu mpendwa mbadilishie Kazi Makonda.

Gwajima : Makonda hajatumwa na Rais kufanya anayoyafanya

Gwajima : mimi namfahamu vizuri Rais, hawezi kumtuma Makonda kufanya hivi.

Gwajima : Makonda atavuka mipaka sasa, atakemea Polisi, atakemea jeshi, atakemea wabunge

Gwajima : Makonda atakemea mpaka waziri mkuu.

Gwajima; wenzetu wabunge wameungana kutumia sheria na kanuni zao watamuhoji.

Gwajima : sisi raia wa kawaida tusio na sheria wala kanuni za kututetea tutashtaki wapi? .

==>Msikilize Hapo Chini Akiogea

WEMA SEPETU AKIRI KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

MAGOLI 10 BORA AFCON 2017

Friday, 20 January 2017

MASHABIKI SIMBA, YANGA WANAOMINI UPUUZI NA UZUSHI NDIYO MBINU ZA KUSAIDIA TIMU ZAO

UKIFUATILIA vizuri utakuta mashabiki wa Yanga na Simba wamekuwa msitari wa mbele sana kulalamikia waandishi wakitumia neno “kuandika vibaya”.
Mashabiki wengi wamekuwa wakilalamika kwamba timu au klabu zao zinaandikwa vibaya pale kunapokuwa kuna jambo ambalo haliwafurahishi.

Wanatumia neno kuandikwa vibaya kwa kuwa tu timu au klabu imekosolewa. Mashabiki hupenda kuona kila kitu kinachoandikwa kwao kinakuwa ni sifa tu.

Huenda wangefurahia na kuliamini au kulipenda gazeti, redio au runinga inayotangaza kuhusiana na sifa zao tu. Watakaokosoa wataonekana wanaandika “vibaya” na chuki ndiyo itatangulia baina yao na chombo au mwandishi husika.

Nimeshuhudia maisha hayo kwa zaidi ya miaka 18 ndani ya uandishi wa michezo. Lawama za kijinga kabisa za mashabiki ambazo zimekuwa hazina msingi hata kidogo.

Wako mashabiki ambao hupenda kuonekana mbele ya wenzao wana uchungu sana na klabu, tena wakataka kumzodoa, kumuudhi au kumtengenezea mwandishi kashfa ili waonekane wameumia sana. Lakini hawajui wanafanya upuuzi mwingi usio na kipimo.

Ajabu, baada ya miaka mingi ya utamaduni huo wa kutaka kuandikwa “vizuri”, sasa baadhi ya mashabiki wa Yanga na Simba wametengeneza mizizi ya kuandikana “vibaya” wenyewe kwa wenyewe.
Wanaitumia mitandao ambako kila mtu ni mwandishi. Kila anayeweza kusoma na kuandika ni mwandishi, hakuna anayeona kwamba uandishi ni kitu kigumu kwake.

Kumezuka tabia mbaya, ya kijinga iliyojaa upuuzi ambayo inapaswa kukemewa kwa nguvu zote tena Yanga na Simba hasa wale mashabiki wengi wanaojitambua, waizungumze kwa kuikemea wakiiona kama ugonjwa hatari ambao ukiachiwa na kukua basi mwisho itakuwa ni tatizo kubwa sana.

Wapo mashabiki wa Yanga, wamekuwa na tabia kila mara kuandika mambo kadhaa, wakayageuza kama vile ni habari ambayo imetolewa na chombo fulani cha habari kikizungumzia Simba. Mfano juzi, waliandika eti “BREAKING NEWS: Simba imetangaza kumfukuza kocha wake, Joseph Omog, hii ni baada ya Simba kufungwa na Azam FC kwenye fainali ya Mapinduzi.”

Mpuuzi aliyeiandika akapewa sapoti na rafiki zake wengine wapuuzi zaidi. Mara moja wakaanza kuisambaza mitandaoni wakijua wazi wanafanya kitu cha kipuuzi ambacho kinaweza kufanywa na wendawazimu tena wasiojitambua.

Lakini siku chache kabla, kuna shabiki mpuuzi wa Simba, yeye aliandika makala uchwara ambayo ilikuwa inaonyesha gazeti la Championi lilifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye alikuwa ameamua kujiondoa kutokana na hali kuwa mbaya.

Utaona sasa, mwandishi uchwara kama huyo akililisha maneno gazeti kwa makusudi kwa kuwa ana uwezo tu wa kuandika A, B, C, D….na kadhalika. Tena watu hawa wanaona sawa na kutoka katika makundi kadhaa ya mitandao hasa WhatsApp nao wanawaunga mkono kuthibitisha upuuzi uliotukuka kutoka ndani ya fikra mbovu walizonazo.

Mtindo huu wa kijinga lazima utakuwa umeanzishwa na baadhi ya mashabiki wajinga wa Yanga na Simba. Ninaamini wao hawajui kipimo cha ujinga wao, ndiyo maana wanaona sahihi kusambaza ujinga huku wakijua ni ujinga.

Kuwaunga mkono ni kuwa mjinga zaidi yao. Kuona wanafanya sahihi ni kuwa juha kabisa, maana ni zaidi ya ujinga.

Ushauri wangu, acheni vyombo vya habari vifanye kazi yake. Kama una kitu cha kuandika basi vizuri kama unakosoa, kuwa huru. Unataka kuhabarisha na unaona ni jambo sahihi, fanya hivyo.

Lakini kuandika jambo la uongo, ukijua ni uongo na kulisambaza, ni uendawazimu uliotukuka. Kama kweli mnaweza kuwakosoa waandishi wanafanya jambo fulani si sahihi, vipi leo uongo unakuwa ni kitu cha kawaida? Huu ni ujinga uliopindukia.

Mimi bila ya woga, nakemea, napinga na nitaendelea kupingana nao bila ya kujali waandishi hao hewa mitandaoni ni kina nani, wana nguvu gani na nikiwajua siku moja nitawaanika kwa majina na picha zao na kuwakemea kwamba ni watu wa hovyo walio na mawazo ya hovyo wenye sifa ya kuitwa majuha.

AISHI MANULA AANDIKA REKODI YAKE, SASA DAKIKA 630 BILA YA KUFUNGWA HATA BAO MOJA

Suluhu waliyoipata Azam, juzi Jumatano dhidi ya Mbeya City, imemfanya kipa wa Azam, Aishi Manula, kucheza mechi saba mfululizo ambazo ni sawa na dakika 630 bila ya kuruhusu wavu wake kutikiswa.

Manula ambaye anasifika kwa uhodari wa kuokoa mikwaju ya penalti, amefanikiwa kufanya hivyo katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Mapinduzi.

Mara ya mwisho kwake kuruhusu bao ilikuwa ni Desemba 24, mwaka jana kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.

Baada ya hapo, akaiongoza Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons, kisha kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi matokeo yalikuwa hivi; Azam 1-0 Zimamoto, Azam 0-0 Jamhuri, Azam 4-0 Yanga, Azam 1-0 Taifa Jang'ombe na Azam 1-0 Simba.

Manula anatakiwa kufanya hivyo kwenye mechi nne zijazo ili kuipiku rekodi ya Muivory Coast, Vincent Angban ambaye kabla ya kuvunjiwa mkataba na Simba, msimu huu alicheza mechi kumi za kimashindano bila ya kuruhusu bao.

SIMBU AWASHUKURU DSTV, WATANZANIA, WAZIRI NAPE AWEKA NENO LAKE




Mshindi wa mashindano ya Mumbai Marathon ambaye ni balozi maalum wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Alphonce Felix Simbu, amewashukuru Watanzania kwa kuendelea kumsapoti na amewaomba kwa pamoja washirikiane kuitangaza nchi kimataifa.

Simbu ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kumpongeza iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Hafla hiyo imekuja baada ya Jumapili ya wiki iliyopita Simba kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mbio za Mumbai Marathon zilizofanyika India na kuwabwaga Wakenya na Waethiopia walioshika nafasi ya pili mpaka kumi.

“Kama mlifuatilia zile mbio, katika kumi bora, kulikuwa na Wakenya saba na Waethiopia wawili, huku Mtanzania nikiwa peke yangu, kama nisingejitahidi basi Tanzania tusingekuwa na furaha kama hii.

“Hivyo niombe tu tushirikiane wakati mwingine tuandae wanariadha wengi ili kuwa na nafasi kubwa ya kushinda, naamini tukifanya hivyo nchi yetu itakuwa juu ndani ya kipindi kifupi,” alisema Simbu.  

Wakati huohuo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alisema: “Nichukue fursa hii kumpongeza shujaa wetu Simbu na Kampuni ya Multichoice kwa kuitangaza nchi kimataifa, ushindi ulioletwa na Simbu ni mkubwa na umeitangaza Tanzania.

“Serikali peke yake haiwezi kufanikisha hili, hivyo nitoe wito kwa makampuni binafsi kuja kwetu tushirikiane kuwekeza katika vipaji kama hivi, tunataka siku zijazo tuwe na mashujaa wengi kama Simbu, isiwe tu kwenye michezo, bali hata katika muziki na sanaa mbalimbali, naamini dunia itatutambua vilivyo.”


Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, alisema wataendelea kumdhamini Simbu, na wanataka awe chachu na hamasa kwa vijana wanaochipukia ili waone kweli kila kitu kinawezekana, kikubwa ni kujituma tu.