IBADA YA SIKU YA
JUMAPILI UFUFUO NA
UZIMA ARUSHA.
SNP FRANK
SOMO:
FUNGUO ZA UFALME 24/9/17.
MATHAYO 16;19
Kwenye serikali ya Mungu tumepewa uwezo wa kufungua lolote
na uwezo wa kufungua lolote ufalme wa Mungu upo kwa ajili ya wana wa Mungu
,serikali ipo kwaajili ya kutatua kero mbalimbali za wanadamu.
Tunaandaa vitu mbalimbali kwaajili ya uchaguzi,pia serikali
ipo kwa sababuba ya kutatua kero zao wanaohitaji misaada.
Pia Mungu nae ana
serikali kwaajili ya wana wa mungu kwaajili ya kusaidia kero mbalimbali za watu
wa Bwana,wewe unatakiwa upeleke kero kwenye serikali ya Mungu ambayo iko ndani
yako,na wewe uliyeokoka unakuwa raia kwenye ufalme wa Mungu.
Ninyi sio raia wa hapa duniani ndio mana mna chukiwa ndio
mana hampendwi,kwanini uko jinsi ulivyo kwa sababu ufalme wa Mungu uko ndani
yako pia ufunguo wa kufungulia lolote uko ndani yako,watu hatujajua kuutumia
ufalme wetu,kwa hiyo wafuga majini wachawi wale wote ni watoto wa giza au wana
wa ufalme wa giza,kwa hiyo wanapokuja kumtesa mwana wa Mungu Inakuwa
haieleweki,
Sisi watoto wa Mungu tunayomipaka ya kuwaamuru wakuu wa giza
ambao hawataweza kuja kwangu bila kukaguliwa mipakani wewe ni raia kwenye
serikali ya Mungu ,wachawi hawana mamlaka wakija lazima wauliozwe na walinzi
wako ambao ni Malaika watakatifu wa Bwana mana wewe ni raia wa ufalme wa Mungu
na kondoo wa malisho yake.
Kuna vitu maalumu ambavyo vimeandaliwa na Bwana kwaaajili ya wampendao Mungu amewaandalia
watoto wake,pia anasema nimekuandalia mambo hapana wa kuzuia ,kwenye ulimwengu
war oho kuna stoo ya Baraka za mtoto wa Mungu.
kwa kanuni ya Mungu, Mungu huandaa mahitaji kabla hajamleta
mlengwa kwenye mahitaji yake ndio maana Mungu kabla hajamuumba Adamu alianza
kwanza kumuandalia mahali ambapo atakuja kuishi.
MWANZO 2:8 na 15 na pia Waefeso 1;3 inazungumzia kuhusiana
na Baraka ambazo Bwana ametubarikia
Kule mbinguni kuna chumba cha Baraka za kila mmoja ambapo siku ukifika mbinguni utaonyeshwa na utabaki unashangaa, ni kwanini hapa
duniani ulikuwa unahangaika,Yesu anawaambia msisumbukie mle ninyi wala mnywe
nini,angalie baba yenu Wa mbinguni anawalisha ndege wa angani ambao hawana hata
mashamba wala maghala ya chakula,Je nyinyi si bora kuliko hao ndenge wa angani?
Maombi Pokea
funguo za Baraka zako pokea kwa jina la
yesu.
Tatizo sio Mungu tatizo hujafungua wewe mwenyewe,Maisha yako
maana Yesu alishatupa unguo wa ufalme lakini watu wengi hawajajua namna ya
kuutumia huo ufunguo.
MATHAYO 16:19
Kuna vitu vyako vimefungwa mahali na wakuu wa anga, wakuu wa
giza ,mizimu,mashetani,wachawi,waganga wa kienyeji na majeshi ya pepo wabaya
kwenye ulimwengu wa roho.
kwenye kila kizazi kinachoendelea kuna waamaleki wanaozuia
usiende kwenye Baraka zako,waamaleki ni watoto wa mtu mmoja anaitwa Esau,wana
wa Israeli ni watoto wa Yakobo tunaona
watoto wa Esau wamekuwa na vita wanawazuia watoto wa ndugu yake yakobo wasiende
kule ambako Mungu alitaka waende kwenye Baraka zao,kile kitendo cha kuwazuia
kule Mungu alipotaka waende,tunaona Bwana ameapa atakuwa na vita na waamaleki.
MWANZO 36;16-12
Kuna vita pia inaendelea lazima uinuke kupigana
nao,wameshaona mahali unapotakiwa kuingia kwenye Baraka zako.
Kuingia ndani ya Baraka sio tatizo, tatizo hujajua kutumia
Baraka zako,ufalme wa Mungu ni kama gari ambalo mtu akifungua anaanza kutumia
kuliendesha gari lake,kuna namna ya kufungua na namna ya kutumia hizo barakan
zako.
kwenye kufungua Baraka zako lazima upigane vita unapigana
ukiwa hapa duniani,Bwana ameapa atakuwa na vita anaefanya vita juu yako Bwana
atamfutilia mbali
Bwana akamwambia Musa nina hasira na waamaleki,waamaleki wamesimama
kinyume na mapenzi ya Mungu,akamwambia Musa mwambie Yoshua ashuke bondeni akapigane
na waamaleki,lazima ushuke mwenyewe kupigana vita kwaaajili ya Baraka
zako,kufungua mlango kunahitaji vita.
KUTOKA 17;8
Waamaleki wakatokea kuwapinga wana wa Mungu ,ule upinzani
unaokupinga usiende kwenye Baraka zako ndio vita yako,maisha yana sehemu mbili,
unaingia kufungua maisha yako lakini watu
wana kuzuia usiweze kuingia kwenye Baraka zako.
Ufunguo ni mamlaka ya kumpinga shetani ukiwa vitani kwaajili
ya kufungua njia pia unatakiwa kuwa mlimani na mikono iwe juu ili ushinde
vita,mwamuzi wa kushinda vita kw wana wa Israeli alikuwa ni Musa lakini aliyefanikisha huo ushindi alikuwa Mungu.
Kutoka Misri kwenda Kaanani ilikuwa ni safari ya siku tatu lakini wana wa Israeli waliogopa
kuipita njia amabayo ingewafikisha kwenye nchi ya ahadi kwa muda wa siku tatu
kutokana na kuwa njia hiyo ilikuwa ikikaliwa na wafilisti na badala yake
waliamua kupita njia ambayo iliwagharimu miaka arobaini kuifikia nchi ya ahadi
.
kuogopa vita unachelewa kufika kwenye nchi yako ambayo Bwana
amekuandalia.
MAOMBI ;Katika
jina la yesu nakwenda kinyume na wasimamizi wa laana ili usifikie nchi yako ya
ahadi kutoka kwa Bwana ninavunjavunja hiyo laana kwa jina la yesu.
Usipopigana itakuchukua muda mrefu kuyafikia mafanikio yako,kuogopa
vita na mikono kuwa milegevu ni hatari kwa mafanikio yako,Bwana alimwambia
kalebu nimekupa wewe mlima huu uwe urithi wako na watoto wako.
YOSHUA
14;6
Musa akaniapia akisema hakika nchi utakayo kanyaga itakuwa
ni nchi yako,kuna Baraka zako zimekaliwa na kiriadhiaba ukiogopa vita
unachelewa kumiliki Baraka zako,unapoogopa kupigana vita unachelewesha pia
watoto wako .
Vita unayoiogopa kupigana nayo leo watoto wako watakuja
kuipigana,usiposhinda vita leo unawapa shida watoto wako.
Kwahiyo unapoogopa kupigana unachelewa kumiliki,tunaona wana
wa Israeli walichele kumiliki kwa kuwa njia yao ilikaliwa na wafilisti.
MAOMBI;Kila
mfilisti uliyekalia njia yangu leo
nakufuata nakubomoa achia kwa jina la Yesu,ewe kiliadhiaba unayeshikilia maisha yangu nakuja na ufunguo
wa ufalme kuufungua mambo yangu kwa jina la yesu.
Pokea ushindi kwa jina la yesu lazima utengeneze mlango wa
Baraka kwa ajili ya uzao wako, miliki ukiwa unanguvu kwa jina la Yesu.
Ukichoka unampa shetani nafasi ya kukupiga
2.SAMWELI 17;1
Mikono ya Daudi ilipochoka Daudi alipigwa.
Mungu amekupa Baraka ila hataki umiliki kizembe,tunaona Adama
alipewa bustani ambayo ilikuwa na kila kitu ndani yake lakini Mungu alimwambia ailime na kuitunza ,maamuzi ya kushinda yako
mikononi mwako kuna wakati unatakiwa kwenda kwenye uwanja wa vita na kuna wakati
unakuja mlimani.
Kuna pepo la usingizi linakuwa linakuja na kukuletea
usingizi wakati unapotaka kuanza kupigana vita yako hivyo ni lazima uwe mkakamavu,
usikubali kulala kiroho kwa jina la yesu,ukichoka adui anapanda magugu.
MAOMBI;kila
magugu nang’oa kwa jina la yesu.
Yesu ametupa mamlaka
ya kukanyanga nyoka na ng’e na
nguvu zote za Yule muovu ibilisi na hakuna kitakachotudhulu .